Bidhaa

Bidhaa ya kwanza ya Daktari itakuwa ni Daktari CD4. Daktari CD4 ni mfumo wa kuhesabu idadi ya seli ya CD4. Mfumo huu wa Daktari CD4 unatumia chombo imara na kinachoweza kubebeka kwa urahisi na kutumika kila mahali, kutoka ofisini mwa daktari hadi sehemu mbali na zenye upungufu wa kiteknolojia. Mfumo wa Daktari CD4 unaunganisha ugunduzi wa kiteknolojia wa aina ya ‘Microscale’, urahisi wa umbo na utumiaji. Hizi sifa zinawezesha Daktari CD4 kuleta umuhimu wa vipimo vya damu kwa sehemu za ulimwengu ambapo mamilioni ya watu sasa wanapata madawa ya kuokoa maisha, lakini hawawezi kupata matibabu bora kutokana na uchunguzi duni.

Kwa kweli, Teknolojia ya Daktari ni rahisi kwa dhana na kutumia (utumiaji) kama mita ya sukari. Hii inatoa vikwazo viwili muhimu kwa kupima hatua-ya-huduma: maandalizi tata ya sampuli na vihisi tete vya macho vilivyo ghali.

Microfluidics – Teknolojia ya uandalizi wa sampuli za Dakatri, inayojulikana kwa wataalamu kama ‘microfluidic cell chromatography’, hutenganisha seli na chembechembe zingine katika chumba kidogo cha kuhisi bila kutumia ‘paipeti’, vitambulisho au vitendanishi vya aina vyo vyote. Pia hii teknolojia haina hatua tata za mwongozo zenye huchukua vipimo vya damu nje ya mikono ya wanakliniki wanaofanya kazi mbali na maabara ya kisasa.
Electrochemical Sensing- Daktari CD4 pia inajinufaisha na ugunduzi wa pili wa,’lysate impedance spectroscopy’. Mfumo huu unatumia kifaa cha kuhisi ambacho uhesabu seli za CD4 zilizotekwa kwa kupima yaliyomo ndani ya seli hizi kwa kutumia umeme. Chombo cha mkono kinatumika kuifasiri ishara ya umeme, na hupeana ripoti ya idadi ya seli za CD4 baada ya dakika chache.

Kwa kuwa hazina shida za lensi, kamera, na vinyunyuzi au vifaa tata za macho ambazo huhinda vipimo vya uchunguzi kwa zahanati, vituo vya afya , na walezi mkono; Daktari CD4 itaweka uwezo wa matokeo sahihi ya upimaji mbalimbali katika mikono ya watu ambao wanayoyahitaji . Kwa sasa Daktari CD4 inaendelezwa na kukadiriwa jinsi inavyofanya kazi.