
Bodi Ya Ushauri
RRashid Bashir ni Abel Bliss Profesa wa Umeme na uhandisi wa Tarakilishi na biolojia, katika Chuo Kikuu cha Illinois, Urbana-Champaign, ambapo pia yeye ni Mkurugenzi wa Maabara ya Micro na Teknolojia ya Nano. Yeye ni mwanzilishi wa teknolojia ya bioMEMS, vihisi vya hatua-ya -huduma, na Teknolojia ya Nano kwa matumizi ya matibabu. Moja ya nia yake ni kuunganisha uhandisi na biolojia kutoka hali ya chembechembe mbalimbali hadi tishu ndogondogo, na matumizi ya semikondakta kwa uhandisi wa matibabu, ili kutatua matatizo ya matibabu. Alisaidia katika uundaji wa mfumo wa umeme ambao ni msingi wa teknolojia ya Daktari CD4. Pia yeye ni mwandishi au mwandishi mwenza wa majarida zaidi ya 100, magazeti ya mikutano 120, na amepewa hataza (patent) 33. Yeye ni mwanachama wa IEEE na AIMBE.
Xuanhong Cheng amekuwa Profesa msaidizi wa P.C. Rossin wa uhandisi wa biolojia na Material Science’ katika Chuo Kikuu cha Lehigh tangu 2008. Yeye ana PhD katika uhandisi wa biolojia kutoka Chuo Kikuu cha Washington na alishirikiana katika uundaji wa ‘microchip’ ya Daktari CD4. Pendeleo lake kwa utafiti wa jumla ni katika kuendeleza ‘microfluidic platforms’ ya kutengeneza sampuli za kibiolojia na kuzigundua chembechembe za biolojia, hasa kuundwa kwa teknolojia za kufaa utambuzi wa huduma.
Mehmet Toner ni Helen Andrus Benedict Profesa wa Upasuaji (uhandisi wa biolojia) katika Hospitali ya Massachusetts General Hospital, Harvard Medical School. Yeye mwanzilishi wa kukuza vyombo vya clinical microfluidic na mifumo ya microelectromechanical yenye matumizi pana katika tiba na afya duniani. Pia Mehmet ni mshiriki katika uundaji wa microchip ya Daktari CD4 na ni mwanzilishi wa kampuni kadhaa za bioteknolojia. Yeye ni mwandishi wa majarida ya kisayansi na kiufundi zaidi ya zaidi 250, ni muunzi wa hataza zaidi ya 30, na ana shahada ya PhD kutoka MIT.