Bodi Ya Wakurugenzi

Roger Kitterman analeta ujuzi wa zaidi ya miaka 15 kwa Daktari wa kuwekeza kwa mradi wa huduma za afya, ikiwa ni pamoja na mshiriki msimamiaji katika mashirika ya Mi3 Venture Partners, na Lee Munder Venture Partners. Shirika la Mi3 Venture Partners liko katika hatua ya kwanza ya kulenga hazina ya uhandisi wa kibiolojia. Kwa sasa, Roger ni mshiriki wa Partners Innovation Fund, na ni mwanzilishi wa “Mass Medical Angels”. Roger ana shahada la MBA ya Fedha na Maendeleo ya Kibiashara kutoka Shule ya Biashara ya Columbia na AB kutoka Harvard College.
Stanley Lapidus ni mjasiriamali mwenye uzoefu. Yeye alianzisha na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa makampuni tatu ya umma, Cytyc, Exact Sayansi, na Helicos BioSciences. Kwa sasa Stanley ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya SynapDx Corp, ambayo alianzisha mwaka wa 2009 ili kuendeleza uchunguzi mpya wa ugonjwa wa autism ( ugonjwa wa akili wa watoto). Pia yeye hufunza katika Programu ya Biomedical Enterprise – Chuo Kikuu cha MIT na ni mbuni wa hataza (patents) 31 za Marekani.
Ed Roberts ni Profesa katika MIT Sloan School of Management, mwanzilishi na mwenyekiti wa “MIT Entrepreneurship Center”, na mwanzilishi aliye na ujuzi mwingi, mwekezaji na mjumbe wa bodi katika makampuni mbalimbali ya teknolojia ya juu yanayoanza. Makampuni penye Ed anajigulisha kwa sasa na hivi karibuni ni pamoja na “Advanced Magnetics”, “Inverness Medical’, “Meditech, Pegasystems’, “Sohu.com”, na Visible Measures. Pia, Ed ni mwandishi wa vitabu kadhaa juu ya teknolojia na ujasiriamali, na ana shahada nne kutoka chuo kikuu cha MIT, ikiwa ni pamoja na PhD ya Uchumi.
Bill Rodriguez ni mMwanzilishi na Mkurugenzi Mkuu wa Daktari Mchunguzi.
Aaron Sandoski ni mkurugenzi mkuu katika Norwich Ventures. Awali, Aaron alifanya na DEKA, jumuiya ya washauri mabingwa ya Dean Kamen, ambapo alisaidia kuendeleza ushirikiano na kubuni mipango ya biashara za teknolojia zinazojitokeza. Aaron alianza kazi yake kama mshauri katika McKinsey & Company, ambapo alishauri wateja wa huduma ya afya wakiwemo makampuni yanayoongoza kwa vifaa vya kutibu hadi mahospitali katika sehemu za mashambani. Aaron alipata shahada la MBA kutoka Shule ya Biashara ya Harvard na kufuzu kutoka Chuo kikuu cha Dartmouth na shahada mbili za AB katika Kemia na Uchumi.

Comments are closed.