Menejimenti

Bill Rodriguez – Mkurugenzi Mkuu
Bill amekuwa kiongozi katika afya ya kimataifa kwa zaidi ya miongo miwili. Utaalamu wake, umemfanya kuwa mshauri wa thamani wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Bill and Melinda Gates foundation pamoja na serikali kadhaa za Afrika na Asia. Kati ya mwaka wa 2003 na mwaka wa 2007 yeye alikuwa Afisa Mkuu wa Maswala ya matibabu katika shirika la ‘Clinton Foundation’. Kwa wakati huo, aliwajibika kubuni na kuendeleza mkakati na masoko ya bidhaa za afya ya kimataifa na sera za kliniki na programu. Yeye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Brown na Shule ya Tiba katika Chuo Kikuu cha Yale.
Aaron Oppenheimer – Makamu wa Rais wa Kubuni na Kukuza Bidhaa
Aaron ana ujuzi wa zaidi ya miaka 20 kwa kubuni na kuendeleza bidhaa. Hapo awali, alifanya kazi katika shirika la Hewlett Packard sehemu ya bidhaa ya matibabu. Kwa wakati huo alikuwa na jukumu la kubuni sehemu ya uhusiano na watumizi ya mfumo wa kufuatilia wagonjwa. Huu mfumo umebaki kiwango cha sekta ya matibabu. Kisha alifanya kazi karibu muongo mmoja kama mshauri wa kubuni na kukuza bidhaa za ‘sayansi ya maisha’ / ‘lifescience’ kwa wateja wakiwemo mashirika ya Dade-Behring, Insulet, na Respironics, pamoja na bidhaa zitumiwazo kwa makumpuni ya Samsung, General Motors, na OXO.
Robert Etheredge, Ph.D. – VP Operations (Makamu Uendeshaji / Utendaji)
Rob analeta ujuzi wa karibu miaka 25 kwa Daktari wa kuendeleza, kuzalisha katika viwanda, na kudhibiti ubora wa vyombo za matibabu. Awali aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Uendeshaji katika kampuni ya “Transport Pharmaceuticals”, ambapo aliongoza uhandisi na uundaji wa kifaa cha kuwasilisha (kutoa) dawa iliyokuwa na gharama nafuu ya uzalishaji katika viwanda kwa wingi wa mamilioni ya vitengo kwa mwaka. Awali, Rob alifanya kazi kwa miaka kumi kama Mkuu wa Kampuni ya Arthur D. Little, Inc, na kama Mwanasayansi Mkuu katika kampuni ya Tyco International.

Comments are closed.